Je wewe ni mwandishi na ungependa maandiko yako yatokee na kuonekana kupitia www.kiumeni.com?
Kiumeni.com inakaribisha maandiko kutoka kwa waandishi wa chini na juu yenye kuhusu mambo yanayowazunguka jamii ya kiume na kupokea mawazo, fikra pamoja na maono tofauti tofauti.
Na tungependa kupokea maandiko juu ya maono yafuatayo;
- Mawazo Pevu ya Ujasiliamali,
- Dondoo za maendeleo,
- Mapenzi, Hisia na Mahusiano,
- Fasheni,
- Mawazo Pevu ya kibiashara.
- Kubadilishana mawazo na wanaume wengine.
- Kukuza kipaji chako na kufanya ujulikane zaidi na kusaidia kuongeza ujuzi kwenye fani ya uandishi.
- Maeleze machache kuhusu wewe yatachapishwa chini ya maandiko yako ili ujulikane kwa wasomaji.
- Maandiko unayoandika yanatakiwa kuwa asilimia 100% mawazo yako na yawe ya kipekee.
- Maandiko yote yawe ni kuhusu mambo yanayowazunguka Wanaume na si vinginevyo.
- Maandiko yote yanatakiwa kuwa na faida kwa wasomaji wote wa jinsia ya Kiume.
- Hakuna maandiko yoyote yatakayolipiwa, yote yatakua kwa faida ya uandishi, kuongeza ujuzi na kufahamika.
- Kama una blog au website, unaweza kuandika maandiko na kupachika link inayoelekea kwenye blog au website yako, pamoja na link nyingine inayoelekea kwenye profile yako ya mtandao wa jamii.
- Maandiko yote yatakua yanalekebishwa ili yaeleweke zaidi na kuwekewa staili.
- Tungependa ushee maandiko yako na watu wako ulionao kwenye mtandao wa kijamii.
- Tunahaki ya kubadilisha masharti ya uandishi wakati wowote.
waulizewanaume@gmail.com
Kuwa chanzo, onyesha maono na dira kwa jamii ikuzungukayo.
Kuwa Mwanaume Mtanashati.
COMMENTS