Karibu Kiumeni, kila mtu huwa anajiuliza ni jinsi gani ya kuondoa mafuta tumboni, iwe tumbo ni la kati au ni kitambi kimejitokeza. Kwa mwili mnene wenye mafuta mengi ni vigumu kuona matokeo mazuri ya kuridhisha kwa kufanya mazoezi pekee, maana asilimia hamsini ya mafuta mwilini huifadhiwa chini ya ngozi, na kiasi kingine kilicho baki huwa ndani ya misuli. Kufanya mazoezi ya mwili pekee hakuwezi kuondoa mafuta hayo mwilini.
Hauitaji kuingia gharama au kuumia sana ili upunguze tumbo, unachohitaji kujua ni vitu vichache kuhusu mwili wa binadamu!.
Karibu Kiumeni, kila mtu huwa anajiuliza ni jinsi gani ya kuondoa mafuta
tumboni, iwe tumbo ni la kati au ni kitambi kimejitokeza. Kwa mwili mnene wenye
mafuta mengi ni vigumu kuona matokeo mazuri ya kuridhisha kwa kufanya mazoezi
pekee, maana asilimia hamsini ya mafuta mwilini huifadhiwa chini ya ngozi, na
kiasi kingine kilicho baki huwa ndani ya misuli. Kufanya mazoezi ya mwili pekee
hakuwezi kuondoa mafuta hayo mwilini.
Mtu mnene akifanya mazoezi ya kuvuta tumbo hawezi kuona
matokeo, hata kama akirudia mazoezi hayo mara mamia kwa siku, kitakachotokea ni
kweli ataimalisha misuli yake ya tumbo ila
hatoweza kuona matokeo hayo kwa sababu tumbo bado litakuwa limezungukwa
na mafuta.
JINSI YA KUPUNGUZA MAFUTA
Kuna usemi unaosema, kwa matokeo ya mazoezi unahitaji.. “ASILIMIA
70 DAYATI, ASILIMIA 30 ZOEZI!”. Kwa matokeo mazuri na ya haraka njia hii hutoa
matokeo mazuri Zaidi tofauti na kupiga mazoezi pekee ambapo ni kweli unaweza
kuwa unaumguza mafuta mwilini ila hauwezi kuunguza mafuta yakutosheleza kwa
siku kuweza kuonyesha matokeo mazuri ya mazoezi unayopiga.
Ila kwa njia ambayo itakupa matokeo ya muda mrefu maara
nyingi huwa ni ya kufanya mazoezi kwa muda mrefu, na matokeo haya nayaita ya
muda mrefu maana mazoezi hayo yatakufanya uwe na adabu ya kubadilisha mwenendo
wa maisha yako na kuutunza mwili wako kwa heshima.
Njia ya 70 kwa 30 inatoa matokeo mazuri maana asilimia 70 ya
upunguaji wa mafuta mwilini hufanywa na dayati ya kuangalia nini cha kula na
kipi cha kuondoa kabisa kwenye mlo wako wa kila siku. Hata hivyo kwa kuangalia
dayati pekee haiwezi kukupa matokeo mazuri, maana tafiti mbali mbali za
kisayansi juu ya kupunguza mafuta mwilini zimeonyesha huwezi kupunguza mafuta
mwilini kwa dayati pekee na kupata mwili wa kuvutia pasipo kufanya aina yeyote
ya mazoezi ya mwili, ukitaka mwili uliopungua kwa mpangilio na mvuto lazima
uhusishe pia mazoezi ya mwili.
Njia kuu ya kupunguza mafuta kwa njia ya dayati ni
kupangilia milo yako ya siku, iwapo ukitaka kujua ni chakula gani kitakachokupa
matokeo mazuri Zaidi bonyeza hapa.
Lazima ujue mlo wako utaupangilia katika hali gani, kwa
mfano badala ya kula ovyo hovyo, unatakiwa upangilie milo yako kwa kula kiasi,
kama umezoea kujaza tumbo wakati wa kula, jaribu kushusha mlo wako uwe unakula
kwa kuondoa njaa kwa kuupa mwili vile virutubisho unavyovihitaji tu, na unaweza kula milo mitatu
mpaka mitano kwa siku na usizidishe zaidi ya hapo.
Hakikisha unakula mlo kamili ila kwa kuhakikisha huli vyakula
vilivyotengenezwa kwa sukari, na zingatia kuachana na milo inayotayarishwa kwa haraka, (fast sood) kama chipsi, vitafunwa na vinginevyo vinavyohusiana na
hivyo, zingatia kula vyakula vyenye protini na milo yako iwe kamili na hasa pendelea kula mboga mboga.
Kwa kuzingatia dayati na kwa
kufanya mazoezi yanayohusisha kuchemsha mwili wako kwa kuongeza mapigo ya moyo zaidi utafanya mwili wako ubadilike na kupata matokeo unayo yahitaji,
maana kwa kadri mwili wako unavyochemka ndivyo unavyozidi kuchoma mafuta
mwilini, na kwa jinsi mwili wako unavyopunguza mafuta utafanya ngozi yako
kukakamaa na kufanya mwili wako kupata shepu, kwa hiyo kitu cha kufanya ni
kukazania mazoezi yanayoongeza mapigo ya moyo na kusababisha upumuaji wa
haraka, fanya mazoezi hayo mara tano kwa wiki, bofya hapa kwa maelezo zaidi.
Mazoezi yote unayofanya hakikisha yanahusisha sehemu zote za
mwili kuanzia misuli ya mikono, nyonga, mgongo, mapaja, misuli ya chini ya
miguu na sehemu zote za mwili kwa ujumla.
COMMENTS