Fahamu na jua siri inayomuongoza Mjasiriamali mwenye mafanikio.

Mjasiriamali ni mtu yeyote aliyefungua biashara ya aina yeyote ambae ni mjasiri wa kufanya maamuzi ya kibiashara ili kumuongezea kipato chake kwa faida na maendeleo. Ili kufanya vizuri na kufanikiwa katika ujasiriamali lazima ufahamu na ujue siri inayomuongoza mjasiriamali kama zifuatazo...

      Je unayajua haya majina, Reginald Mengi (IPP Group), Said Salim Bakhresa (Bakhresa Group of companies), Mohammed Dewji (Mohammed Enterprises Tanzania Limited)...?


Watu hawa wana kitu kimoja tu kinacho waunganisha, ni wajasiriamali waliofanikiwa kwa khali ya juu zaidi Tanzania, wameanza ujasiliamali kutoka khali ndogo na kuujijenga katika ujasiriamali na kuwa moja kati ya wajasiriamali wakubwa zaidi Tanzania, ni watu wenye mioyo mikubwa ambao hawarudishwi nyuma kwa upinzani utokanao na maisha kiujumla katika kazi zao, na wameweza kutoa matokeo mazuri zaidi kutoka kwa kile sisi wengine tunachoweza sema "Hakiwezekani!", na wamejitengenezea utajiri mkubwa zaidi ambao na sie tungeweza kujitengenezea kama tu tungeweza kujifunga mikanda mioyo yetu na kufanya kile kinachotakiwa kufanywa na kuachana na mambo yanayotuvunja moyo na kuturudisha nyuma na kusingizia hatuna bahati.

              Hakuna njia pana inayoweza kutuongezea kipato kama sio ujasiriamali, iwapo ukitaka ikutoe kweli kimaisha na kuwa mjasiriamali lazima ujue kipi ufanye ili ufungue mafanikio yako kimaisha na kiuchumi.
              Mjasiriamali ni mtu yeyote aliyefungua biashara ya aina yeyote ambae ni mjasiri wa kufanya maamuzi ya kibiashara ili kumuongezea kipato chake kwa faida na maendeleo. Ili kufanya vizuri na kufanikiwa katika ujasiriamali lazima ufahamu na ujue siri inayomuongoza mjasiriamali kama zifuatazo...
  • Fanya kazi kwa bidii... 
 Kazi kwa bidii ndo injini inayoendesha ujasiriamali, muulize mjasiriamali yeyote kuhusu siri kubwa ya ujasiriamali, jibu la kwanza ni fanya kazi kwa bidii, bidii yako ndo itakuongezea masirahi, kwa kuongeza biashara yako iwe na mzunguko mkubwa zaidi, biashara kama biashara lazima ifunguliwe kila siku na lazima uwahi kufungua asubuhi, kwa hio bidii yako ya kuamka na kuendeleza biashara yako ndio itakayopanua wigo wa biashara yako.
  • Lijue soko lako....     
Ukinunua bidhaa kwa lengo la kuuza lazima ujue utauzia wapi, na utamuuzia nani!, kulijua soko ndo ujasiriamali wenyewe, lazima uumize akili kujua wapi bidhaa gani utaiuza kwa wingi na wapi utakosa kabisa wateja, Mjasiriamali hutumia akili kutafuta soko ili kupanua mzunguko wake wa biashara.
  • Kuwa na mawazo mapya... 
Sio uwone jirani kafungua biashara furani na wewe ukurupuke kuikimbilia, watu wengi wanashindwa kuendesha biashara sababu ya kuiga mambo, anakuwa hana ufahamu mpana na biashara aliyoianzisha na kumfanya asiwe na ujanja wowote mambo yakienda kombo, usiige ni vizuri ukakaa chini ufikirie kipi unafanya, na unakifanyaje.
  • Tumia mikopo kwa usahihi....
Ugumu wa mkopo sio kupokea Hela, ugumu wa mkopo ni marejesho, kama ulianza biashara kwa mtaji wa mkopo, basi hakikisha unafanya marejesho kwa mda uliopangwa, na faida ya biashara usiitumie kwa mambo yeyote ambayo hayakua kwenye mpangilio, ili uweze kuizungusha hio hela na kuzalisha faida zaidi.
  • Kuwa na marengo ya biashara yako...
Biashara bila kuwa na marengo itabaki inazungukia hapo hapo, lazima uwe na marengo, faida ikitoka ujue inatakiwa kwenda wapi, hii itakufanya uweze kutumia faida kujijenga mwenyewe kiuchumi, na huwezi kuwa na marengo wakati hujui unatengeneza faida kiasi gani, lazima upige hesabu na uijue biashara yako kama inaleta faida ama hasara na hapo ndipo utakapo jua marengo yatafikiwa au la!.
  • Kukopesha ni adui wa ujasiriamali...
Ukikopesha katika biashara yako ndo unachochea uchimbaji wa kaburi la kuzikia biashara yako, kukopesha kunasababisha kuyumbisha mtaji wa biashara, maana hela inayozunguka ndani ya mtaji itakua ni ndogo sababu hela nyingi ipo nje umekopesha, hii inasababisha biashara kuyumba na haitochukua mda itakufa.
  • Kuwa mbunifu na mshindani...
Tafuta njia mbalimbali zitakazofanya uongeze mauzo katika biashara yako, mauzo yakiongezeka ndivyo hivyo hivyo faida nayo inaongezeka, fanya matangazo na kuwa mbunifu na mshindani kwa kutafuta njia mbadala za kuongeza mauzo.
  • Kuwa na uelewa mkubwa na bidhaa unayoiuza...
Uelewa na bidhaa unayoiuza itakufanya ulijue soko ndani na nje ya eneo unalouzia, hii itakufanya uipate bidhaa unayoiuza kwa bei inayotakiwa, na hata kama ukiipata kwa bei ya chini hii itakupa faida zaidi.
                   Mjasiriamali ni mtu anayejua biashara hua nzuri au mbaya kulingana na kipindi kilichopo, na anawezo wa kuyatumia yote hayo kujinufaisha yeye pamoja na biashara yake kwa kutengeneza faida zaidi.

COMMENTS

Jobstanzania
Name

Fasheni,3,Jua Zaidi,10,Mahusiano,19,Mazoezi,4,Mchezaji wa Mapenzi,22,Picha Maneno,14,Slider,6,Top Stories,12,WaulizeWanaume,3,
ltr
item
Kiumeni - WaulizeWanaume.: Fahamu na jua siri inayomuongoza Mjasiriamali mwenye mafanikio.
Fahamu na jua siri inayomuongoza Mjasiriamali mwenye mafanikio.
Mjasiriamali ni mtu yeyote aliyefungua biashara ya aina yeyote ambae ni mjasiri wa kufanya maamuzi ya kibiashara ili kumuongezea kipato chake kwa faida na maendeleo. Ili kufanya vizuri na kufanikiwa katika ujasiriamali lazima ufahamu na ujue siri inayomuongoza mjasiriamali kama zifuatazo...
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiNqikuNfFrvFiI_Y5uWg8KCWWWi44EOhYjEH09sfhlYSB3U87sm3N_PguioQpWJMQVYR_oUGI5ag2m3SuA61IMFjkLivRd5KlPjzcOS6RRN5yUdghgs7J96sks7EBj-Y3HZXfL3OGQpTM/s1600/Ujasiriamali(2).jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiNqikuNfFrvFiI_Y5uWg8KCWWWi44EOhYjEH09sfhlYSB3U87sm3N_PguioQpWJMQVYR_oUGI5ag2m3SuA61IMFjkLivRd5KlPjzcOS6RRN5yUdghgs7J96sks7EBj-Y3HZXfL3OGQpTM/s72-c/Ujasiriamali(2).jpg
Kiumeni - WaulizeWanaume.
https://waulizewanaume.blogspot.com/2014/03/fahamu-na-jua-siri-inayomuongoza.html
https://waulizewanaume.blogspot.com/
http://waulizewanaume.blogspot.com/
http://waulizewanaume.blogspot.com/2014/03/fahamu-na-jua-siri-inayomuongoza.html
true
5715942833127633596
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy