Maumivu ya sehemu ya chini ya mgongo au lumbago ni hali inayotokea mara nyingi kwenye hali inayohusu misuli na mifupa ya mgongo. Hali hii huathiri takriban 40% ya watu kwa wakati fulani maishani mwao. Maumivu ya sehemu ya chini ya mgongo yanaweza kuainishwa kwa urefu kama maumivu makali ya ghafla (yanayodumu kwa kipindi cha chini ya wiki 6),maumivu sugu ya wastani (wiki 6 hadi 12), au maumivu sugu (zaidi ya wiki 12). Hali hii pia inaweza kuainishwa kulingana na visababishi kama inayosababishwa na jeraha au isiyosababishwa na jeraha au maumivu hame .
Maumivu ya sehemu ya chini ya mgongo au lumbago ni hali inayotokea mara nyingi kwenye hali inayohusu misuli na mifupa ya mgongo. Hali hii huathiri takriban 40% ya watu kwa wakati fulani maishani mwao. Maumivu ya sehemu ya chini ya mgongo yanaweza kuainishwa kwa urefu kama maumivu makali ya ghafla (yanayodumu kwa kipindi cha chini ya wiki 6),maumivu sugu ya wastani (wiki 6 hadi 12), au maumivu sugu (zaidi ya wiki 12). Hali hii pia inaweza kuainishwa kulingana na visababishi kama inayosababishwa na jeraha au isiyosababishwa na jeraha au maumivu hame .
Katika visa
vingi vya maumivu ya mgongo, kisababishi maalum kikuu hakitambuliwi wala
kukadiriwa, kwa sababu maumivu huaminika kusababishwa na jeraha kama vile misuli
au mkazo wa viunga. Ikiwa maumivu hayapona baada ya kutibiwa kwa njia
isiyohusisha upasuaji au ikiwa maumivu yataandamana na "tahadhari"
kama vile kupungua uzito bila sababu, homa, au matatizo makuu ya kihisia au
mwenendo, uchunguzi zaidi unaweza kuhitajika kubaini kisababishi kikuu. Mara
nyingi, vifaa vya utambuzi kama matumizi ya pichatiba kuchunguza maumivu ya
mgongo yameongezeka. Baadhi ya maumivu ya sehemu ya chini ya mgongo
husababishwa na kuharibika kwa diski za baina ya pingili za uti wa mgongo, na
uchunguzi wa kunyoosha mguu ni muhimu katika kubaini visa hivi. Katika watu
wenye maumivu sugu, mfumo wa mwili unaochakata maumivu unaweza kutofanya kazi
vyema.
Matibabu ya
maumivu ya ghafla ya mgongo kwa kawaida huwa ni tiba isiyohusisha upasuaji,
kama vile vituliza maumivu na kuendeleza kazi za kawaida jinsi mtu anavyoweza
licha ya maumivu. Matibabu hupendekezwa kwa kipindi ambapo yanamsaidia mtu,
huku dawa aina ya acetaminophen (pia inayojulikana kama paracetamol) ikiwa ya
kwanza kupendekezwa. Dalili za maumivu ya sehemu ya chini ya mgongo hufifia
baada ya wiki chache, huku 40 - 90% ya watu wakipata nafuu kabisa baada ya wiki
sita.
Ishara na Dalili
Katika dalili
za kawaida za maumivu ya sehemu ya chini ya mgongo, maumivu haunza baada ya
mwendo unaohusisha kunyanyua vitu, kujipinda au kuinama. Dalili za hali hii
zinaweza kuanza baada ya mwendo wowote au mtu anapoamka asubuhi inayofuata.
Maelezo ya dalili hizi yanaweza kuwa maumivu katika sehemu fulani au maumivu
yanayosambaa. Maumivu yanaweza kutokuwa makali kufuatia shughuli kama vile
kuinua miguu, au hali zingine kama kuketi au kusimama. Maumivu yanayosambaa
chini ya miguu (yanayojulikana kama maumivu ya nyonga) yanaweza kuwepo. Visa
vya kwanza vya maumivu makali ya ghafla ya mgongo huanza katika umri wa miaka
20-40. Mara nyingi kisa hiki huwa ni sababu ya kwanza katika watu wazima
kumwona daktari.
Kisababishi
Maumivu ya sehemu ya chini ya mgongo si ugonjwa bali ni
hali inayoweza kusababishwa na matatizo mengi yanayotofuatana kwa kiwango na
hatari. Visa vingi vya maumivu ya mgongo havina kisababishi maalum, ingawa
vinaaminika kutokana na maswala ya misuli au mifupa kama vile kuteguka aumkazo
wa misuli. Unene wa kupindukia, kuvuta sigara, kunenepa wakati wa ujauzito,
mfadhaiko, matatizo ya mwili, mkao mbaya na kulala vibaya pia huchangia maumivu
ya mgongo.
Udhibiti wa mwili
Imependekezwa
kuongeza mazoezi ya kiujumla ya mwili, lakini hakuna uhusiano bayana
uliotambulika kati ya mazoezi haya na maumivu au ulemavu yanapotumika kama
matibabu ya maumivu ya ghafla. Tafiti za kiwango cha chini hadi za kiwango cha
juu zimependekeza kutembea kama njia ya kutibu maumivu ya ghafla.
Maumivu yakizidi muone Daktari.
SOURCE: Wikipedia.
COMMENTS