"Xperia Z1s, simu ya kampuni ya Sony isiyo ingiliwa na maji" Iliyotoka Januari 22, 2014. Xperia Z1s ni simu isiyoingiza maj...
"Xperia Z1s, simu ya kampuni ya Sony isiyo ingiliwa na maji"
Iliyotoka Januari 22, 2014. Xperia Z1s ni simu isiyoingiza maji ambayo unaweza kwenda nayo kuanzia bafuni mpaka bichi kuogelea au kufanya kitu chochote kinachohusiana na maji, inauwezo wa kukaa ndani ya maji yenye kina cha futi 4.9 kwa muda wa nusu saa. Kampuni ya soni wanawahimiza wateja wake wanaotumia hii simu wawe wanaitumia kupigia picha chini ya maji kwa kutumia kitufe cha nje cha kamera cha simu hio, simu hii inatumia tekenolojia ya mguso na inauwezo wa kuhisi mguso hata kama imeloana na kioo kinateleza.
Xperia Z1s camera ina megapixel 20.7 ambayo inaongezewa nguvu na software za kutosha za kamera na inaweza piga picha na kufanya picha ing'ae huku sehemu za nyuma ya picha zikiwa hazionejani vizuri ili picha itoke kwa uzuri na mg'ao zaidi.
Soni imeweza kuifanya simu iwe ya kijamii zaidi huku ikiendana na mitandao ya kijamii kama facebook na mtumiaji wa simu anaweza kurekodi video huku ikionekana moja kwa moja kwenye kurasa za mitandao jamii kama facebook saa hio hio jinsi na kama anavyoichukua na mtu akikomenti kwenye kurasa ya kijamii basi komenti hio itaonekana moja kwa moja kwenye kioo cha picha ya kamera.
Simu hio ya kampuni ya soni inamuingiliano na playstation 4 ambapo inaweza kutumika kama srini ya ziada au kama limoti kontroo ya playstation 4, simu wakati inanunuliwa inakuja na magemu ya play station mobile yakiwa jumla kumi.
Sifa ya simu hii ni kama zifuatazo...
- Qualcomm snapdragon 800 processor ikiwa na 2.2 Ghz QuadCore CPU
- Ram ya 2gb
- Battery ya 3000 mAh
- Android 4.3 Jelly Bean
- Kamera yenye 20.7 Megapixels, aperture F2.0, focal lenght 27mm (wide angle), 3x clear image zoom, max.ISO 6400, steady shot, HDR ya picha na video, kamera ya mbele ikiwa na 2MP.
COMMENTS