Msongo wa mawazo ndo kitu kinachomtokea mara nyingi zaidi na mara kwa mara kwa binadamu mtu mzima, ndo maana kuna misemo kama, "Mtu mzima ni jalala la matatizo", na kwenye matatizo yanakuja mawazo... na mawazo ya kisongamana ndo msongo wenyewe wa mawazo, sababu za msongo wa mawazo hutofautiana kutoka mtu na mtu, kama msongo wa mawazo unavyoharibu maisha yetu na kufanya tusifikirie vizuri ndivyo hivyo hivyo kinachotokea hata kwenye miili yetu, na kufanya mifumo ya mwili kudhurika kwa hali ya juu kama ifuatavyo...
"Kama Waswahili wasemavyo, Hasira... Hasara!, Cheka uongeze siku."
Msongo wa mawazo ndo kitu kinachomtokea mara nyingi zaidi na mara kwa mara kwa binadamu mtu mzima, ndo maana kuna misemo kama, "Mtu mzima ni jalala la matatizo", na kwenye matatizo yanakuja mawazo... na mawazo ya kisongamana ndo msongo wenyewe wa mawazo, sababu za msongo wa mawazo hutofautiana kutoka mtu na mtu, kama msongo wa mawazo unavyoharibu maisha yetu na kufanya tusifikirie vizuri ndivyo hivyo hivyo kinachotokea hata kwenye miili yetu, na kufanya mifumo ya mwili kudhurika kwa hali ya juu kama ifuatavyo...
Ukiwa na msongo kimwili au kiakili, mwili hubadilisha nguvu zake na kuzielekeza kwenye mfumo wa kupigana, huhisi kuna tatizo kimwili ambalo linatakiwa kupambana nalo na kusababisha ushilikiano wa mfumo wa neva kutuma taarifa kwenye tezi ya adreno kutoa homoni ya adrenaline na cortisol, homoni hizi husababisha moyo kwenda mbio, presha ya damu kuongezeka, kasi ya mfumo wa umeng'enyo wa chakula nayo kuongezeka
pamoja na kuongeza kiasi cha glukosi(sukari) kwenye milija ya damu, hali hii inayosababishwa na msongo huisha mara baada ya hali ya msongo(stress) kwisha.
Kukiwa na msongo(stress), misuli hupanuka, mvuto wa misuli kwa muda mrefu husababisha uchovu, maumivu, kuumwa kichwa au kipanda uso na athari nyingi nyinginezo.
Msongo(stress) hufanya mtu kutopumua vizuri
kwa kusababisha upumuaji wa kasi ambao husababisha mshituko wa maumivu ya kifua kubana kwa baadhi ya watu.
Msongo wa hali ya juu husababisha mapigo ya moyo kwenda mbio, misuli ya moyo kuvutika na mishipa inayopeleka damu kwenye misuli mikubwa na moyo kusinyaa na kusababisha kujaa kwa damu inayotakiwa kusambazwa sehemu hizi za mwili, kuruddia rudia kwa msongo wa hali ya juu husababisha kuvimba kwa mishipa hivyo kutokea kwa ugonjwa wa moyo.
- Mfumo wa homoni endocrini
Endocrini ni homoni nzinazomwagwa moja kwa moja kwenye damu
, mwili ukiwa kwenye msongo sehemu ya ubongo inayoitwa hypothalamus hutuma taalifa na kusababisha tezi ya adeno kutengeneza homoni ya cortisol pamoja na epinephrine ambayo wakati mwingine huitwa "homoni ya msongo'.
INI
Baada ya homoni ya cortisol na epinephrine kutolewa, ini hutengeneza glukosi(sukari) kwa wingi, sukari hii huenda moja kwa moja damuni na kutumika kuupa nguvu mwili kwa ajili ya dharura.
Kwa baadhi ya watu msongo hufanya mtu kula zaidi au kutokupata hamu ya chakula tofauti na ilivyo kawaida, msongo unaweza kukusababisha ule chakula tofauti tofauti au uvute sigara kwa wigi
, au uzidishe utumiaji wa pombe na vileo na kukufanya uzulike kwa kiungulia, au tumbo kujaa gesi, tumbo linaweza kupata maumivu au kutapika pindi msongo ukiwa katika hali ya juu sana.
Kwa wanaume, homoni nyingi ya cortisol inayotolewa kwa shindikizo la msongo huathiri ufanyaji kazi wa kawaida wa mfumo wa uzalishaji, msongo wa hali ya juu husababisha homoni ya testosterone kutokufanya kazi vizuri na kusababisha utengenezaji wa shahawa kuwa mdogo ambao huleteleza ugumba wa muda.
Kwa wanawake msongo husababisha kuingia mara kwa mara kwenye hedhi na tarehe kutokua za uhakika za kuingia kwenye siku zao au kusababisha tumbo la hedhi kuuma sana na kupunguza hamu ya kufanya mapenzi.
COMMENTS