Hamna kitu kibaya kama kuwa na msichana au mwanamke asiyekufahamu, asie kujua kitabia, asie endana na wewe, asiejua chochote kuhusu wewe...
Hamna kitu kibaya kama kuwa na msichana au mwanamke asiyekufahamu, asie kujua kitabia, asie endana na wewe, asiejua chochote kuhusu wewe kwa sababu tu saa zote yupo bize kujua ni nini kifuatacho unachotakiwa umtimizie, yeye anajali yeye pekee na sio kwamba anakuwa hakupendi ila ni nafsi flani ya uchoyo, ya kujiangalia mwenyewe na kujisahau anayokuwa nayo ambayo tabia kama hizi huanza kutokea baadae sana kwenye mahusiano ambapo tayari unakuwa umeshakolea kwenye mapenzi, kwa ufupi mnakuwa hamuendani kitabia.
Nyie wawili msipoendana kitabia japo mapenzi kati yenu yapo sawa kutasababisha tofauti kati yenu, mnakuwa kama pande mbili zinazopingana, huyu anataka hiki na yule anataka kile, ugomvi unakuwa hauwishi na hali ya maelewano kwa jinsi muda unavyokwenda inakuwa ni ngumu,
Kama unataka msichana mzuri unaeendana nae, anaeweza kukujali na kukupeti peti kwa kukupa moyo pale mambo yanapoenda kombo bila kujiangalia yeye mwenyewe kasimamia wapi, mpenzi anayeweza kukujali bila kuweka roho ya choyo au sababu ya umimi, ni muhimu kumjua na kufahamu jinsi ya kutambua tabia ya mwanamke kwa haraka hasa pale mapenzi yanapokuwa machanga kabla hata tabia zenyewe hazijaanza kujitokeza,
Siku zote kiumeni.com ipo kukujuza na baada ya utafiti wa kina kwa marefu na mapana na kuzungumza na wanaume mbalimbali majanga kama haya yamewasibu na wengine wanaendelea kutapa tapa tumekuandalia sababu za kugundua tabia za mpenzi wako mapema ili uweze kujua kwa kutumia akili yako mwenyewe iwapo mtaendana au La.
1, Pima kama anawaongelea vizuri watu wengine...
Iwapo anaongea ovyo kuhusu watu wengine na haoni mazuri watu wanayoyafanya, sidhani kama baadae nawe ukianza kumchukiza kama atakuchukulia poa, kama iwapo anawaongelea vyema wanaomzunguka hata kama ukimtega kwa baya la mtu flani yeye anakubadilisha kwa zuri basi ujue hamna msichana atakayetokea kumzidi, mlinde kama ua rozi linavyolindwa na miba yake.
2, Kuwa chonjo kuangalia jinsi anavyowamudu watu...
Kwa mfano mnapokuwa mmetoka out jinsi anavyo mmudu muhudumu, kama ni kazini jinsi anavyoingiliana na wafanyakazi wenzie, ustaarabu, upole na subira ni nguzo kuu za mke wa kukufanya uzeeke na tabasamu bado unalo mdomoni.
3, Muulize ni kitu gani anachokijali kwenye maisha...
Kama majibu yake atayaweka katika vigezo vya umaarufu na utajiri basi usimtegemee sana kuwepo hali yako ya kimaisha ikidondoka japo maisha ni kupanda na kushuka, iwapo akikujibu anapenda uaminifu, ukweli, uwazi na afya bora basi ujue huyo ni mtunzaji na atapenda sana iwapo mwanaume mwenye mapenzi ya kweli na anayeyaonyesha kuwa pembeni yake.
4, Hakikisha upo katika hali ya utulivu, ukawaida wako...
Hii ni ya umuhimu kabisa maana ili uweze kumfanya mwanamke aanze kuyaongelea haya anatakiwa asikushitukie kuwa unamchimba, kwa hio kabla hujaanza stori hizi jaribu kutafuta sababu za kuziunganishia kwa ndani ndani humo jamaa, iwapo katika tabia zake akionyesha kutokujari, kutokutishwa, chuki na udharirishaji basi jua hata baadae ndivyo jinsi atakavyokuwa akiwa chini ya msukumu flani wa kimaisha unaomsababishia msongo wa kimawazo.
5, Jaribu kufahamu kama mwelewa wa kuomba msamaha na kukiri kukosea...
Kama hana uwezo wa kuomba msamaha na kujua amekosea pale anapokosea basi ujue gharika litakalokuijia na majanga, watu wa namna hii huwa ni wale wanaojisikia ambao kwao huwa hawawezi kujishusha na kujisahihisha pale anapokosea, kwa ufupi ni pasua kichwa.
6, Angalia jinsi anavyokuwa akiwa na mawazo au matatizo...
Bado anakuwa katika hali ya utulivu, mwenye matumaini huku akitafuta njia ya kuyatatua kwa moyo wenye kuyapa nafasi kuwa matatizo yataisha, akiwa hivyo basi nenda katoe mahari mara moja ndo umekutana na mkewe mtarajiwa. Iwapo akiwa mtoa lawama, mwenye hasira, mwenye maneno ya udharirishaji, ndivyo atakavyokuwa hata kwenye maisha yake ya baadae na wewe, na ukitaka kujua mke wa aina hii ana majanga gani kaulize wazee nyumbani watakupasha habari, watakupa hadithi ya yule mama mjane pale mtaani kwenu mumewe aliekufa kwa presha.
7, Kuwa makini anapoongea, maana wengi hujisahau na kuanza kuzungumzia tabia zao bila kujielewa wanafanya hivyo...
Hii ni kwa sababu watu wengi akilini huwa wanaona tabia zao zipo sawa kabisa na hujikuta wanajiongelea kwa kujisifia japo kuwa tabia hizo huwa zina aina flani ya udharirishaji, uchoyo, hasira, zenye uelewa mdogo, kujiona hadhi ya juu, kujikweza na nyingine nyingi bila kutambua kasoro zao.
COMMENTS