Hivi hii rangi inaendana? Rangi ya shati gani inaendana na hii sururali? Maswali haya yanayochanganya na kuumiza kichwa, maswali ya rangi gani inaendana na ipi hutesa akili ya kila mwanaume mtanashati aliyepo sehemu yoyote dunia.
Hivi hii rangi inaendana? Rangi ya shati gani inaendana na hii sururali? Maswali haya yanayochanganya na kuumiza kichwa, maswali ya rangi gani inaendana na ipi hutesa akili ya kila mwanaume mtanashati aliyepo sehemu yoyote dunia.
Watanashati ili kufuzu sanaa ya uvaaji, lazima tuwe wanafunzi tunaohitaji kuelewa kanuni za upangiliaji wa rangi, kujifunza kumechisha rangi si vigumu kama unavyoweza kufikilia, unachotakiwa kujua ni kanuni tu za upangiliaji wa rangi, kujua rangi gani inaendana na ipi.
Kiumeni.com imekuandalia kanuni 5 za msingi za kupangilia rangi ili uvaaji wa nguo zako upendeze kwa hali ya kuongeza mvuto wa taswira yako.
1. Shati jeupe linaendana na kila rangi ya nguo. Pale kila kitu kinaposhindikana nyanyua rangi nyeupe, shati jeupe hendana na kila rangi ya kila nguo uliyonayo. Hasa rangi ya zile nguo ambazo huwa unashindwa jinsi ya kuzipangilia na nguo nyingine, unaweza kuivaa na tai ya rangi ya mistari mistari kama unataka kuvaa tai, au unaweza kuvaa pamoja na sweta lenye kola ya V. Kwa vyovyote vile utatoka bomba na kutokelezea kwa utanashati zaidi.
Shati jeupe linaloendana na mwili wako ni moja kati ya nguo ambazo haziwezi kutoka kwenye wakati na umuhimu wake ni kama dhahabu na kwa mwanaume yeyote mtanashati unapaswa kuwa nayo.
2. Rangi ya Ugoro inaendana na rangi yeyote ile angavu. Kama una nguo ambayo rangi yake ni ya mng'ao na kuwaka sana, ivae na nguo ya ugoro. Ni rangi nzuri ya kupunguza ukali wa rangi nyingine, kwa hio kama unataka kufanya majaribio ya kuvaa rangi yeyote jaribu kuichanganya na rangi ya ugoro na utaona jinsi utakavyotokelezea. Tumia nguo yeyote ya ugoro iwe sweta, suruali au hata jaketi ili kupunguza mgao wa vazi jingine ulilolivaa.
Rangi ya ugoro ni rangi nzuri, yenye wepesi wa kuchanganyika na rangi nyingine ya nguo na ni rangi ambayo haiishi kuendana na wakati.
3. Usivae suruali au nguo yoyote ya chini yenye mng'ao wa kupitiliza. Hata kama uwe nani hakikisha unapinga hamu yeyote ya kuvaa nguo ya chini ambayo inatengeneza mng'ao, iwe ni suruali ya kitambaa, jinzi au nguo yeyote.
Hakikisha chochote unachokivaa chini kisiwe na rangi angavu ya kushitua kuliko shati au tisheti uliyoivaa, suruali ndio msingi wa uvaaji nguo, siku zote inatakiwa isiwe na rangi kushinda rangi ya nguo ya juu uliyoivaa.
4. Vaa nguo zenye mng'ao wa kuendana pamoja. Ili uweze kutokelezea vizuri zaidi kwa mvuto zaidi, hakikisha thamani ya rangi ziwe zinaendana, nikiongelea thamani ya rangi namaanisha mng'ao wa nguo uwe unaendana, kama umevaa suruali rangi butu ambayo haing'ai basi na shati lazima vile vile iwe rangi butu ambayo haing'ai, na kama vile vile umevaa rangi ya kung'aa, hakikisha pia rangi fuatilizi iwe na mng'ao, Hii haimaanishi ndio uvae rangi zote ziwe na mng'ao wa kupitiliza, hapa tunazungumzia uzito wa rangi.
5. Vaa kwa kuendana na rangi zinazo shabihiana. Fanya usifike njia nzima unayotembea kwa kuvaa rangi zinazoshabihiana, rangi zinazoshabihiana ni rangi ambazo zinapingana kwenye duara la rangi, kwa mfano Nyekundu na kijani, njano na zambarawe, bluu na rangi ya machungwa.
Ukipangilia nguo zako kwa kufatilia rangi zinazoshabihiana kama zinavyoonekana kwenye duara la rangi ndivyo utakavyopendeza zaidi, rangi zinazoshabihiana huletakujiamini na kukufanya uonekane kama mvaaji anaejua nguo na kufahamu rangi na kuzivaa kuendana na mpangilio wa jinsi unavyotakiwa na muonekano makini zaidi.
Kuvaa kwa kufuatana na mpangilio wa rangi ni changamoto kubwa kama hauna ufahamu wa rangi, ila jambo linabaki pale pale lazima wote tujue ili muonekano wetu uwe angavu na wakuvutia zaidi. Na hizo ndizo kanuni 5 za msingi, nenda na ujaribu na sifa zikikumwagikia usisite kutoa shukrani kwenye maoni hapo chini.
COMMENTS