Mapenzi ni Zaidi ya hisia, Zaidi ya kile mpenzi wako anachokiona na kuhisi akuangaliapo, ni jinsi alivyoridhika kwa kila kitu nakukuona wewe upo Zaidi ya jinsi ulivyo, kiasi cha hisia zake kuzidi na kuwa Zaidi ya yeye kuweza kuelezea, kiasi kila akuangaliapo anashindwa kujizuia Zaidi ya kutabasamu.
Mapenzi ni Zaidi ya hisia, Zaidi ya kile mpenzi wako anachokiona na kuhisi akuangaliapo, ni jinsi alivyoridhika kwa kila kitu nakukuona wewe upo Zaidi ya jinsi ulivyo, kiasi cha hisia zake kuzidi na kuwaZaidi ya yeye kuweza kuelezea, kiasi kila akuangaliapo anashindwa kujizuia Zaidi ya kutabasamu.
Kiumeni.com tunachokuambia sio sura yako au swaga zako ndo
zitakazo mfanya msichana akupende Zaidi ya yeye atakavyo, ila ni kwa jinsi wewe
unavyomfanya ajisikie akiwa nawe, jinsi anavyojihisi na kupokea upendo unaotoka
moyoni kwake na kuukubali, ndicho kitu kikuu kitakacho mfanya mpenzi wako
apagawe nawe na kujikuta akikupenda kupitiliza.
Hakikisha kila mda unaotumia nae unamtengenezea kumbukumbu
nzuri, afurahie vitendo mnavyofanya pamoja na kutengeneza historia yenu wawili,
kumbukumbu zinazomburudisha moyo wake kiasi hata ukiwa mbali na akazifikilia,
zinamfanya atabasamu na hisia za kukumisi kumjaa mara dufu, hizo hisia za
kumtaka awe tena karibu yako zimfanye asiache kukutafuta kwenye simu na
kukutumia meseji.
Mfanye ajione tofauti, ajihisi unamwona spesho na sio kwa
sifa unazompa ila kwa jinsi unavyomchukulia, aone kwa vitendo, aamini kwa macho
yake mwenyewe, hii itamfanya akupende bila kujihisi, afanye vitu kwa jinsi
mapenzi yanavyompeleka yeyewe, ajitoe kwa moyo na kukuona kuwa nawe ni bahati
hivyo atajikuta anaitumia hio bahati kwa marefu na mapana, huku akiwa ajiulizi
wala kujishuku.
“mara nyingi wanawake huwa na hofu ya kupenda, hofu ambayoinawatawala Sana na iwapo huwa unawasikiliza kwa makini utakuwa umeshaisikiahofu hii, sababu kuu ya hofu hii ni kuwa, wanawake wanaogopa kutendwa, wanahisiwakimpenda mwanaume kupitiliza, na huyo mwanaume akajua kutamfanya huyomwanamme kumshusha thamani mwanamke”,
Iwapo ukimwondolea hii hofu na kujikutaanakuamini kutamfanya akupende bila mipaka, bila mashaka na kukolea kwenyemapenzi Zaidi na Zaidi na Zaidi.
COMMENTS