Sio kwamba hana hisia, Unasababisha asikutake.

Kwa mwanamke mapenzi ni hisia, hisia za yeye kukuwaza wewe, hisia ya kutaka kukuona kwa sababu hajakuona na anatamani kukuona, hisia ya yeye kuwa na wasiwasi kuhusu mpenzi wake, ukiondoa hicho kitu cha kumfanya akuwaze, basi muda si muda utaanza kumtoka kichwani.

Kuna sehemu kwenye maisha mwanaume kama mwanaume inabidi uwe mwanaume, ujitenganishe kati ya hisia unazojisikia, uweke utofauti kati ya kile kifurushi ulichonacho cha muanguko wa kihisia na ukweli uliopo, ufanye maamuzi sio kwa sababu ya upendo ila kwa sababu ya kutengeneza mazingira ya kiuhalisia kwa mapenzi ulionayo kwa msichana wako.

Kuachana na maamuzi ya presha ambayo moyo huyafanya kwa uwoga wa kumpoteza mpenzi wako, kwa kuhisi mapenzi kwa mpenzi wako yatapungua na kujikuta unafanya kitu ambacho badala ya kuyaweka mapenzi yako na yule umpendae pazuri, yanakufanya uonekane fala na mtu usiekuwa na maamuzi ya msingi na unayepaparuka kwa kuendeshwa nahisia kiasi cha kumfanya msichana wako haisi utofauti juu yako, kwake unakuona unafanya mambo kupitiliza, kiasi cha kuzidi mipaka unaanza kuboa.

Kwa historia na ufahamu, tokea uumbaji wa binadam, mabadiliko ya kibinadam hutokea sababu tu, binadam hubadilika kwa kuangalia mazingira aliopo, sio sababu tu anakurupuka kufanya kitu ili kutimiza mazingira yanavyoitaji, kwa mfano mwingine ua likisinyaa sio kufanya juhudi la kulifanya lisisinyae ila ni kufanya maamuzi ya kulibadilishia mazingira kama udongo na mbolea ili lichanue.

Hata mahusiano ni hivyo, mambo sikuzote lazima yabadilike, zile stori za kupendana sana ipo siku lazima zitaanza kufifia, na ule ukaribu wa kila dakika kutumiana sms ya “Nakumisi”, utabadilika utakuwa wa saa au kwa siku nzingine utakuwa mara moja kwa siku au kutokuwepo kabisa.

Utofauti huu ukianza na ukaanza kuhisia umbali kati yako na msichana wako unaanza kutokea, sio ndo ufikie maamuzi ya kukurupuka na kupagawa, badala ya kuonyesha upendo uliokua nao wa kawaida unaanza kuingiza shauku na kujipa mawazo na wasiwasi ya kuwa upendo wake umepungua, hivyo kwa asilimia kubwa sana kutokana na wasi wako unaanza kuingiza maamuzi ya kuongeza zaidi kiasi cha kumpenda bila wewe kujijua, unajikuta wewe ndo unaanza kupiga simu zaidi kuliko yeye, unaanza kumtumia meseji zaidi hata kabla hajajibu umesha tuma meseji tano.

Unayafanya mapenzi kuanza kuwa ya upande mmoja kwa kutompa pumzi ya kupumua msichana wako, na kusababisha zile hisia alizonazo kwako kuanza kupungua maana unafanya mambo mengi kwake, japo wewe unaona kawaida ila kwake unaanza kumboa maana hata ule mda wa kumfanya yeye akumisi anakua hana tena, ule muda wa kumfanya yeye akuone kimya na kuanza kukuwaza “Hivi anafanya nini sasa hivi, mbona yupo kimya?” anakuwa hana tena maana kila muda wewe unakuwa unammwagikia kwa meseji na simu mpaka anaanza kusahau hisia zake mwenyewe kwako.

Kwa mwanamke mapenzi ni hisia, hisia za yeye kukuwaza wewe, hisia ya kutaka kukuona kwa sababu hajakuona na anatamani kukuona, hisia ya yeye kuwa na wasiwasi kuhusu mpenzi wake, ukiondoa hicho kitu cha kumfanya akuwaze, basi muda si muda utaanza kumtoka kichwani.

Mazoea ya wewe kuwa ndo unamtumia meseji yeye tu kila saa na kila wakati, kutamfanya yeye asiwe anakutumia maana anajua na kutarajia baada ya dakika kadhaa lazima mlio wa sms yako atausikia, hivyo ile hali ya yeye kukuweka kipaumbele inakwisha kwake, na sio sababu anataka iwe hivyo bali wewe ndie unaesababisha, kama ujuavyo “demu akikufata fata na kukusonga kwa kila jambo, hata kama unampenda itafikia kipindi ataanza kukuboa na thamani yake kushuka”, basi hicho pia hutokea upande wa pili wa shilingi iwapo tukiwafatilia kupita kiasi na kutojiamini kwa kuwa wanaume dhabiti..

COMMENTS

Jobstanzania
Name

Fasheni,3,Jua Zaidi,10,Mahusiano,19,Mazoezi,4,Mchezaji wa Mapenzi,22,Picha Maneno,14,Slider,6,Top Stories,12,WaulizeWanaume,3,
ltr
item
Kiumeni - WaulizeWanaume.: Sio kwamba hana hisia, Unasababisha asikutake.
Sio kwamba hana hisia, Unasababisha asikutake.
Kwa mwanamke mapenzi ni hisia, hisia za yeye kukuwaza wewe, hisia ya kutaka kukuona kwa sababu hajakuona na anatamani kukuona, hisia ya yeye kuwa na wasiwasi kuhusu mpenzi wake, ukiondoa hicho kitu cha kumfanya akuwaze, basi muda si muda utaanza kumtoka kichwani.
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhwOMMXSM1AyFhMpqrCN8s2lpozHrYCv0uhL7Ldp7NI7Cl05PK2ngxHtowuOfBX3ZJMUxI81v8UUhnYc2FIRqaZPFCaZ-n8Xq1GDnYR8FSiCQc7effGVgi1nO9zzIZuQ8OrAkNTXc6BWtU/s640/kiumeni.com.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhwOMMXSM1AyFhMpqrCN8s2lpozHrYCv0uhL7Ldp7NI7Cl05PK2ngxHtowuOfBX3ZJMUxI81v8UUhnYc2FIRqaZPFCaZ-n8Xq1GDnYR8FSiCQc7effGVgi1nO9zzIZuQ8OrAkNTXc6BWtU/s72-c/kiumeni.com.jpg
Kiumeni - WaulizeWanaume.
https://waulizewanaume.blogspot.com/2016/02/sio-kwamba-hana-hisia-unasababisha.html
https://waulizewanaume.blogspot.com/
http://waulizewanaume.blogspot.com/
http://waulizewanaume.blogspot.com/2016/02/sio-kwamba-hana-hisia-unasababisha.html
true
5715942833127633596
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy