"Ni watulivu, wanajiamini, wakiingia sehemu kila mtu anasimamisha anachokifanya na kugundua uwepo wao, wakiongea watu wote wengine wanawasikiliza, wengine wanataka kukaa nao wawasikie kile wanachozungumzia na kufanya, wanawake wanataka kutoka nao, hawa ni wanaume viongozi."
"Ni watulivu, wanajiamini, wakiingia sehemu kila mtu anasimamisha anachokifanya na kugundua uwepo wao, wakiongea watu wote wengine wanawasikiliza, wengine wanataka kukaa nao wawasikie kile wanachozungumzia na kufanya, wanawake wanataka kutoka nao, hawa ni wanaume viongozi."
Mwanaume kiongozi anasifa moja ambayo inamtofautisha na mwanaume yeyote yule wa kawaida, yeye ni kiongozi asilia, mkusanyiko wa wanaume wengine unamfata yeye, anaongoza na kuwalinda wote wanaomzunguka.
Dunia ya mabadiliko inampa fursa nyingi mwanaumehuyu kiongozi, wakati wengine wanaona tatizo, mwanaume kiongozi katika asilia yake anaona sababu na athari, na anazibadilisha na kutengeneza fursa kwa jamii imzungukayo, anapenda kushinda na siku zote ndivyo alivyo.
Haupi kipaumbele muonekano wake, anachojari ni kushinda na kufanikiwa kwa kile anachokifanya kwa wakati huo, chochote anachokifanya watu wengine wanamfuata, wengine wanataka wafanane nae, wananakiri mitindo yake, jinsi anavyoongea na muonekano wake, mwanaume kiongozi yeye hufuata mitindo yake mwenyewe na hawezi nakili toka kwa mtu yeyote mwingine.
Mara nyingi anakua ametulia mpaka anapohitajika kufanya jambo, haogopi kupigania kwa kile kinachohitajika na chenye umuhimu na ni kiongozi mzuri wa wanaume aliyepo.
Kuna vitu ambavyo mwanaume kiongozi huwezi kukuta anafanya, Kiumeni.com imejaribu kukusanyia vitu kumi ambavyo iwapo na kama unavifanya basi ni dhahiri wewe sio mwanaume kiongozi.
#10; Unamwachia msichana wako alipie gharama za mtoko.
Mwanaume kiongozi huudumia jopo lake na anawajibika kwa kila kitu, kama mwanamke wake akijitolea kulipa bili, ataichukua bili taratibu na kwa utulivu na kumwambia "niachie mimi", mwisho wa mjadiliano.
#9; Hauombi msamaha hata kama umekosea.
Mwanaume kiongozi hakatishwi kitu, atasema kwa urahisi "Nimekosea nisamehe kwa hilo", na anasawazisha tatizo kama linawezekana.
#8; Unajipendekeza kwa viongozi na kutafuta idhini yao.
Mwanaume kiongozi hajipendekezi kwa mtu, anajiamini na kuamini afanyacho maana yeye ni kiongozi asilia.
#7; Unafanya Umbea.
Unafanya umbea juu ya bosi wako, rafiki zako na wengineo, haujali kuwasonta vidole watu wengine kwa mapungufu na udhaifu wao huku ukichekelea, mwanaume kiongozi hageuzii mgongo wenzake, anawasimamia na kuwaelekeza jinsi ya kufanya mambo na haitaji kujijenga kwa kuwaangusha watu wengine.
#6; Unashituka kwenye majanga na haujiamini.
Mwanaume kiongozi asili yake ni mabadiliko na kujiamini, na mabadiliko ya kasi ni changamoto nzuri kwake, anapiga hesabu kwa kuangalia sababu na athari na majibu anayoyapata yanampa fursa ya kufanya kitu endelevu na cha muhimu kimaendeleo.
#5; Unafanya mambo bila kufikiri.
Mwanaume kiongozi anafanya mambo kwa kasi, ila anafikilia kwanza kwa umakini mkubwa kabla ya kufanya, hakimbii ovyo ovyo na kukurupuka ila anatumia busara na umakini.
#4; Unatoa lawama kwa wengine.
Mwanaume kiongozi anawajibika kwa matendo anayoyafanya.
#3; Unadangaya.
Unadanganya watu wanaokuzunguka, unamdanganya bosi wako, unadanganya rafiki zako, mwanaume kiongozi sio muongo na anasimamia kile anachoongea na kama ni kitu kimeharibika anawajibika na kufanya kile kilicho sawa.
#2; Unawasaliti wengine ili ufanikiwe.
Mwanaume kiongozi hasaliti watu wake, kama kuna kitu kinamtatiza anamfata mtu anayehusika.
#1; Unawaonea wengine.
Mwanaume kiongozi hupigana pale panapohitajika na penye umuhimu wa kufanya hivyo, hapaparuki na wala kamwe hakurupuki na sio muonevu bali husaidia na kama kunatatizo hulitatua kwa kuwashilikisha wengine pale panapohitajika msaada.
COMMENTS