Unampenda kimapenzi hautaki kumpoteza, ila humuelewi amebadilika.

"Je upo kwenye uhusiano wa mapenzi na mtu maalumu ambaye hutaki kumpoteza?, Je unapata hisia mbaya na unahisi kunakitu hakiko sawa maana kila ukitaka kumbusu mpenzi wako au kukaa nae muongee hana hisia tena kama alizokuanazo awali, kila kitu anakuwa na kisingizio na mizungusho mpaka unapata hisia labda kuna mtu mwingine katikati?".

"Je upo kwenye uhusiano wa mapenzi na mtu maalumu ambaye hutaki kumpoteza?, Je unapata hisia mbaya na unahisi kunakitu hakiko sawa maana kila ukitaka kumbusu mpenzi wako au kukaa nae muongee hana hisia tena kama alizokuanazo awali, kila kitu anakuwa na kisingizio na mizungusho mpaka unapata hisia labda kuna mtu mwingine katikati?".

 Nikitu gani unachokijua ambacho wanaume wanakifanya ila wanawake hawakifanyi?, unajua ni nini?, wanaume hupingana na hali halisi katika sehemu mbili za maisha yao, namba moja; huwa hawaulizi njia inaelekea wapi au mahali walipo pindi wapoteapo njia na namba mbili; huwa wanadhani wanawake wote hawaeleweki wala hawaendani nao.

Watu hawa kamwe huwa hawajiulizi kwanini baadhi ya wanaume wengine huwezi kukuta wamekataliwa na mwanamke au wameachwa na mwanamke, je inawezekana kwamba baadhi ya watu hufanya makosa kwenye mahusiano na makosa hayo hujirudia kutoka uhusiano mmoja kwenda mwingine?, au inawezekana kwamba uchaguzi wa wanawake katika wanaume si dhabiti?

Muongozo; 

Wanaume walio na mafanikio kwenye mapenzi huwa hivyo sio kwa sababu ya bahati, ila ni kutoka na kutumia kanuni za kuaminika na kuwa na mipango thabiti.

Kiumeni.com imekuandalia kanuni thabiti ambayo unatakiwa uifatilie vizuri na kuielewa maana ndo itakuwa nguzo kuu ya mafanikio katika mahusiano yako ya kimapenzi na kukufanyia mabadiliko makubwa ya utanashati.

Kanuni; Kuwa na chamgamoto. 

Hamasa au mvuto wa mwanamke kimapenzi ni kitu cha muhimu sana cha kuangalia iwe wakati unamtongoza mwanamke au uko naye tayari katika mahusiano, wakati unamtongoza hamasa inakuonyesha kiasi cha uhakika ulionao kukubaliwa au kukataliwa, na katika mahusiano huonyesha kiwango cha mvuto wa kimapenzi alichonacho mwanamke juu yako, hamasa hupungua na kuongezeka kutokana na jinsi wewe unavyoendesha mapenzi na mpenzi wako, kanuni kuu ya kuongeza hamasa ni jinsi unavyotoa changamoto kwa mwanamke.

Changamoto ni kitu ambacho wanawake wanakitaka na ndicho kitu pekee kitakachomfanya mwanamke akae kwa muda mrefu, tuchukulie mfano umekutana na msichana mpya na mnaanza kuongea, maongezi yanaendelea na yanazidi kuwa matamu, unaanza kumwelezea kuhusu maisha yako pamoja na mahusiano yako ya kimapenzi yaliyopita, na kumgusia juu ya wapenzi wako wa zamani na mahusiano yako kwa ujumla na kwa jinsi anavyokusikiliza unajua kabisa mpo ukurasa mmoja kwa mambo mengi mnayoyaongea, mpaka kufikia mwisho wa maongezi umeshamwambia kila kitu kuhusu wewe, kwa hio kwa hapo unakua umeshamaliza changamoto yeyote uliokuanayo.

Naposema umeshamaliza changamto namaanisha hutakiwi kuwa muwazi sana, kama kaka yangu Abel anavyosema "Ukiona maongezi yamekolea na anakuangalia kwa jicho la husuda, kinachofuatia ni kuaga ili umwache anakufikilia.

Haimaanishi unampenda kiasi gani, unachotakiwa kuangalia ni kiasi gani upendo wake unavyoongezeka kwako na jinsi anavyoanguka kwenye mapenzi yako, ongoza matendo yako na maongezi yako, hakikisha haumsimulii mambo yako yote, mwache mwenyewe atafute na kufungua kurasa moja hadi nyingine ya maisha yako, kuwa changamoto kwa kumpatia kitu kitakachomfanya akufikilie, mwanaume kiongozi anatambua changamoto ni sehemu kubwa ya mahusiano ambayo kipindi hiki wengi huwa hawazingatii, kwahio kama upo kwenye mahusiano ila unaona msichana wako amebadilika inatokana na kushuka kwa hamasa yake kwako, na hamasa ikishuka sana, tukichukulia hamasa kwa asilimia 0 mpaka 100%, na ikawa imeshuka chini ya asilimia 40% atakua anakuona kama unamboa na ni kitu cha kawaida kwa wanawake maana wanahitaji changamoto kwa wakati wote, na ikishuka sana chini ya asilimia 30% lazima atataka muachane.

Kwahiyo unawezaje kuwa na changamoto muda wote? 

Unachotakiwa kufanya ni kufanya hamasa yake juu yako iwe katika kiwango cha juu muda wate na si vinginevyo, lazima uonyeshe kujiamini na kujiheshimu kwa hio usije pitiliza na kujinadi sana na kitu kimoja naomba ufahamu kujinadi ni kuzuri kwa yule mchekeshaji mwenye uelewa na ujuzi mkubwa na wanawake, na ameshakuwa na wanawake wengi na anachohitaji zaidi ni ngono pekee.

Jiongoze kama mwanaume kiongozi , namaanisha tunza hisia zako na hakikisha zipo chini ya muongozo wako, kama ulikua mtu wa kumuhitaji sana kila muda jaribu kumpa nafasi, kama shemeji yangu anavyosema "Huwezi kukitamani kitu mpaka kipotee", na si maanisha usionyeshe hisia zozote kama jiwe ila weka uwiano na hasa katika mitoko yako ya kwanza.

Kujiheshimu na kujithamini ni sehemu kubwa ya kujiamini, kujithamini ni nguvu chanya na itakupa mwongozo mzuri kwenye uhusiano, kama haujiamini kwanini mtu mwingine akuamini?, tuachane na yote hayo mwisho wa kina ni kwamba muonyeshe mpaka ulipo, ila sio kwa kumwambia.

Kuwa na maamuzi kwenye uhusiano na unatakiwa ufanye maamuzi ambayo na kwako pia yanakunufaisha, na kama unamaamuzi yote kwake basi rafiki hapo ni mteremko tu.

mwanaume kiongozi anajiamini na anajithamini kwa hali ya juu na kufanya maamuzi ndani ya mahusiano kwa umakini zaidi na saa zote anaziongoza hisia zake na kama ukifanya hivi sawa, huyo msichana atakupenda daima na labda ndo atakaevalishwa ile pete.

COMMENTS

Jobstanzania
Name

Fasheni,3,Jua Zaidi,10,Mahusiano,19,Mazoezi,4,Mchezaji wa Mapenzi,22,Picha Maneno,14,Slider,6,Top Stories,12,WaulizeWanaume,3,
ltr
item
Kiumeni - WaulizeWanaume.: Unampenda kimapenzi hautaki kumpoteza, ila humuelewi amebadilika.
Unampenda kimapenzi hautaki kumpoteza, ila humuelewi amebadilika.
"Je upo kwenye uhusiano wa mapenzi na mtu maalumu ambaye hutaki kumpoteza?, Je unapata hisia mbaya na unahisi kunakitu hakiko sawa maana kila ukitaka kumbusu mpenzi wako au kukaa nae muongee hana hisia tena kama alizokuanazo awali, kila kitu anakuwa na kisingizio na mizungusho mpaka unapata hisia labda kuna mtu mwingine katikati?".
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjmpTLQnvvzW9Sf1mpyeQdGY2P-K0H5n3RMFTzXRX6xb9iXHnnf5wErGMKHD40pmYHpqVVjj-2QxFbm4vHAWarRU6RSVb3IBhO9XZuxmKCMbdZR0ATdoOmd-MQ2hkGQZGhC5yamEcA4YTg/s1600/waulzewanaume.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjmpTLQnvvzW9Sf1mpyeQdGY2P-K0H5n3RMFTzXRX6xb9iXHnnf5wErGMKHD40pmYHpqVVjj-2QxFbm4vHAWarRU6RSVb3IBhO9XZuxmKCMbdZR0ATdoOmd-MQ2hkGQZGhC5yamEcA4YTg/s72-c/waulzewanaume.jpg
Kiumeni - WaulizeWanaume.
https://waulizewanaume.blogspot.com/2014/05/unampenda-hautaki-kumpoteza-ila.html
https://waulizewanaume.blogspot.com/
http://waulizewanaume.blogspot.com/
http://waulizewanaume.blogspot.com/2014/05/unampenda-hautaki-kumpoteza-ila.html
true
5715942833127633596
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy