Mambo 8 ya kukumbuka wakati maisha yako yanaenda vibaya na kukosa mwelekeo wenye mafanikio.

Tukienda na ukweli kuwepo kwa furaha kwenye maisha ya mtu haimaanishi ndo ya kuwa mtu huyo huwa hana matatizo, ukiwa katika hali ngumu na ukaona wenzako wanafuraha haimaanishi maisha yao ni mazuri sana kuzidi ya kwako, sema wanakuwa na uwezo mkubwa wa uvumilivu na wanaangalia zaidi kile walichonacho na si vile walivyovipoteza, maisha ni mawimbi hupanda na kushuka, kinachokupasa ni kutokata tamaa na kusonga mbele.

"Siku zote angalia ulichonacho na siyo kile ambacho hauna, kwa sababu siyo kile dunia inachokichukua ndiyo kinachohesabika ila ni kile ulichonacho na jinsi unavyokitumia".

Tukienda na ukweli kuwepo kwa furaha kwenye maisha ya mtu haimaanishi ndo ya kuwa mtu huyo huwa hana matatizo, ukiwa katika hali ngumu na ukaona wenzako wanafuraha haimaanishi maisha yao ni mazuri sana kuzidi ya kwako, sema wanakuwa na uwezo mkubwa wa uvumilivu na wanaangalia zaidi kile walichonacho na si vile walivyovipoteza, maisha ni mawimbi hupanda na kushuka, kinachokupasa ni kutokata tamaa na kusonga mbele.

Siku zote angalia ulichonacho na siyo kile ambacho hauna, kwa sababu siyo kile dunia inachokichukua ndo kinachohesabika ila ni kile ulichonacho na jinsi unavyokitumia.

Kiumeni.com imekuandalia mambo 8 ya kuangalia wakati maisha yakienda kombo na kukufanya kukosa nguvu na hali ya kupigana nayo.

  • #1, Maumivu ni sehemu ya ukuaji.
Saa zingine maisha hukufungia mlango kwa sababu ni muda wa kuendelea kusonga mbele zaidi na hicho ni kitu kizuri maana mara nyingi huwa hatuendelei kusonga mbele mpaka jambo litokee linalotulazimisha kufanya hivyo, maisha yakikubana jikumbushe hakuna maumivu ambayo hutokea bila marengo, jitoe katika sehemu inayokuumiza ila usisahau jambo ambalo maumivu hayo yamekufundisha, kuhangaika kwako hakumaanishi jambo hilo linataka kukushinda bali kila mafanikio makubwa yanahitaji mahangaiko flani ili kufanikishwa.

Kama kiumeni.com tunavyosema mambo mazuri hayahitaji haraka, kuwa mvumilivu na ijenge akili yako kwa mawazo chanya na kila kitu kitakuwa sawa, japo haviwezi kubadilika na kuwa sawa muda huo huo, kuwa na subira lazima yatakuwa sawa.

Kumbuka kuna aina mbili za maumivu, maumivu yanayokuuma na maumivu yanayokujenga na kukubadilisha, ukiwa unaendelea na maisha yako usiyapinge, maumivu yote mawili yatakusaidia ukuwe kimaisha.

  • #2, Kila kitu kwenye maisha ni cha muda mfupi.
Kila mvua inaponyesha hufikia kipindi inakatika, kila unapoumia hufikia kipindi unapona na baada ya giza huja mwangaza na badala ya kuamini ya kuwa giza litakuwepo daima milele badilisha fikra zako na amini kutapambazuka.

Kwa hiyo kama kuna vitu havikuendei sawa sasa hivi, jua matatizo yatapita na mwangaza utakuja. Sio kwa sababu maisha ni magumu ndo yasikufanye usitabasamu, na sio kwa sababu kuna kitu kinakusumbua ndo kisikufanye usicheke, kila kipindi kinakupa fursa mpya na mwisho mwingine, unapata nafasi ya pili ya kujirekebisha mambo yako na makosa yako kwa kila sekunde, unachotakiwa ni kuichukua na kuitumia vizuri.

  • #3, Wasiwasi na lawama haziwezi kubadilisha kitu. 
Wale wanaotoa lawama siku zote huwa hawatimizi jambo kwa manufaa, ni heli kujaribu kufanya kitu kikubwa na kikakushinda badala ya kutokufanya kitu kabisa na kutegemea mafanikio, kupoteza nafasi haimaanishi mambo ndio yamekwisha, mambo huisha pale ambapo haufanyi kitu chochote na bado unalaumu, kama ukiwa unaamini kitu endelea kujaribu na usiogope mambo yaliotokea zamani kuwa yatajirudia na ukayaacha yakuzibie mlango wa maswala yako ya baadae na yanayokuja.

Ukiitumia leo unalaumu kuhusu jana, haitofanya kesho kuwa rahisi na yenye mafanikio, chukua hatua na chukua ulichojifunza na endeleza maisha yako, fanya mabadiliko na usiangalie nyuma.

Kwa chochote kinachotokea, kumbuka furaha ya kweli huanza kuingia pindi unapoacha lawama kuhusu matatizo yako na badala yake kutumia huo muda kuyaelewa na kuelekeza nguvu kuyatatua matatizo yako.

  • #4, Makovu yako ni alama ya ujasiri wako.
Usiyaonee aibu makovu maisha yaliyokuachia, makovu humaanisha maumivu yamekwisha na kidonda kimepona, pia humaanisha umeyashinda maumivu yaliyosababishwa na miangaiko ya maisha yako, hakikisha umejifunza vyema somo ulilopatiwa kutokana na hayo makovu, kuwa mjasiri zaidi na endelea kusonga mbele.
  • #5, Kila mahangaiko unayopitia ni hatua ya kusonga mbele.
Kwenye maisha subira sio kusubiria jambo pekee, ni uwezo wa kuwa na nidhamu isiyo na pupa kutarajia jambo bila haraka huku ukifanya kazi kwa bidii kutimiza ndoto zako, kwa hio ukitaka kujaribu usiangalie muda na fanya jambo kwa juhudi zote hata ikimaanisha kukosa pakuegemea, kuhenya bila matumaini, kutokula vizuri, kutolala vizuri tofauti na ulivyokua umezoea au kutojisikia vizuri, chochote kinachotokea matatizo ni kipimo cha uwezo wa kuyahimili maisha, kuwa na subira na matumaini makubwa kwamba unaweza na utaweza chochote maisha itakachokutupia.
Kama unakitaka hicho kitu lazima utakitimiza ili mradi uwe na husuda pamoja na maamuzi ya kukitaka bila kuangalia na kujali kharaha unazozipata pamoja na mahangaiko unayoyapitia maana ndo hatua zenyewe za kusonga mbele.
  • #6, Kelele za watu wengine zisikufanye wewe kutokuendelea.
Kuwa na mawazo chanya hasa watu wafitini wakiwa wamekuzunguka na kukukatisha moyo kwa kile unachokifanya, usiruhusu mawazo ya mtu mwingine yakuingie na kukukosesha mwelekeo wa mipango yako na kukukatisha tamaa kile moyo wako unachokiona kiko sahihi kufanya, mtu asikuingilie fikra zako, jua msimamo wako na ni matokeo gani unayohitaji kuwa nayo na ni malengo gani uliojipangia.

Ni asili ya watu kuongea, kwa lolote na chochote ufanyacho lazima yupo atakaekuwa na mawazo tofauti na wewe, usiangushwe moyo, kuwa na msimamo na jambo lako.

  • #7, Kama ipo, ipo Tu.
Ujasiri mkubwa hupatikana hasa ukiwa na mengi ya kulilia na kulaumu ukaamua kubadilisha fikra zote hizo kuwa maamuzi dhabiti na nia ya kupata kile unachokihitaji, kuna baraka zilizofichwa kwenye kila mahangaiko unayoyapitia kwani yanakujenga na kukupa uelewa zaidi juu ya nini cha kufanya ila tunachotakiwa ni kufungua macho yetu ili kuziona hizo baraka ambazo hutupatia njia mbadala ya kufanya mambo.

Huwezi lazimisha vitu vitokee ila unaweza kuvisababisha vitokee kwa kufanya mambo kwa nia na juhudi kubwa, hata kama mambo yakienda vibaya ndo uelewa wako unavyozidi kukuwa zaidi juu ya hilo jambo linalokusumbua na kumaanisha utafanya vizuri zaidi mara nyingine maana mafundisho mazuri na muhimu katika maisha huwa tunajifunza wakati maisha yanapokuwa magumu au pindi tunapokua tumefanya makosa katika maisha.

Penda maisha yako, jiamini hasa kwenye mambo yanayokuwa yamegusa maisha yako na amini maamuzi unayokua umeyafanya, amini fikra zako na tumia nafasi vizuri pale zinapojitokeza, usin'gang'anie mambo ila tumia njia mbadala kwa kuyachunguza matatizo yako na kuyaelewa hapo unaweza kuelekeza nguvu zako zote kuyatatua, usitumie papara na kutaka kutumia nguvu kulazimisha kitu kitokee bali kuwa na subira na sababisha jambo kutokea kwa kutumia akili yako ipasavyo badala ya kulazimisha, sawa sawa na ulazimishe hii tivotu iliyokutayarishia haya makala kuitwa waulizewanawake.com wakati kiuhalisia inaitwa kiumeni.com, maana kama ipo ipo tu.

  • #8, Kitu kizuri unachoweza kukifanya ni kuendelea kufanya unachofanya kwa juhudi.
Usiogope kusimama unapoanguka na kujaribu tena, jaribu tena kupenda, jaribu tena kuishi na kuwa na ndoto, usiruhusu maisha magumu yaukaze moyo wako, unapojisikia kutaka kuacha ufanyacho kumbuka mara nyingi mambo huenda vibaya sana kabla hayajawa mazuri, saa nyingine inakubidi upitie mahangaiko magumu ili kufikia neema nzuri yenye mafanikio uyatakayo.

Maisha ni magumu ila wewe ni mgumu zaidi, tafuta nguvu za kucheka kila siku, tafuta ujasiri wa kufanya na kujisikia utofauti wenye kupendeza, tafuta njia kwenye moyo wako kufanya na wengine watabasamu, pia usijipe msongo wa mawazo kwa vitu ambavyo huwezi kuvibadilisha, ishi maisha huru, penda kwa upendo, ongea kwa wema na ukweli, fanya kazi kwa bidii na hata kama mafanikio huyaoni ongeza bidii zaidi na endelea kufanya unachofanya. Endelea kukua.

Kiumeni.com inakupa ushauri wa vitu vya kufanya kila siku asubuhi mara umkapo,
  1. Amka ukiwa na fikra chanya.
  2. Kula kwa afya.
  3. Fanya mazoezi kuulinda mwili wako, kuupa nguvu na kuupendezesha.
  4. Usiwe na wasiwasi sana.
  5. Kuwa na juhudi kwenye kazi na bidii.
  6. Tabasamu na cheka mara kwa mara.
  7. Lala vizuri.
Rudia kila siku kufanya mambo haya.
Uwanja ni wako.
Ni kitu gani kinachokusaidia wakati mambo yako yakienda vibaya?.
Ni fikra gani chanya unayoifikiria kichwani mwako wakati kila kitu kikienda vibaya?.
Toa maoni yako ndani ya kiumeni.com hapo chini na shirikisha mawazo yako kwa watu wengine. 

COMMENTS

Jobstanzania
Name

Fasheni,3,Jua Zaidi,10,Mahusiano,19,Mazoezi,4,Mchezaji wa Mapenzi,22,Picha Maneno,14,Slider,6,Top Stories,12,WaulizeWanaume,3,
ltr
item
Kiumeni - WaulizeWanaume.: Mambo 8 ya kukumbuka wakati maisha yako yanaenda vibaya na kukosa mwelekeo wenye mafanikio.
Mambo 8 ya kukumbuka wakati maisha yako yanaenda vibaya na kukosa mwelekeo wenye mafanikio.
Tukienda na ukweli kuwepo kwa furaha kwenye maisha ya mtu haimaanishi ndo ya kuwa mtu huyo huwa hana matatizo, ukiwa katika hali ngumu na ukaona wenzako wanafuraha haimaanishi maisha yao ni mazuri sana kuzidi ya kwako, sema wanakuwa na uwezo mkubwa wa uvumilivu na wanaangalia zaidi kile walichonacho na si vile walivyovipoteza, maisha ni mawimbi hupanda na kushuka, kinachokupasa ni kutokata tamaa na kusonga mbele.
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjkkp9kJ_V7QMROqATDYNCuJ6AMf3Bt94WYXU2laFqh0N1NQHsqrdBCl8tDa_J9tTMaXzoQ4XHs986QSmr-O4YxgtFaFch7CnGizTOIAHU8zBe6DU329rGok90c3811_GckA7wIGlNYbfU/s1600/139136870_4fadd2f255.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjkkp9kJ_V7QMROqATDYNCuJ6AMf3Bt94WYXU2laFqh0N1NQHsqrdBCl8tDa_J9tTMaXzoQ4XHs986QSmr-O4YxgtFaFch7CnGizTOIAHU8zBe6DU329rGok90c3811_GckA7wIGlNYbfU/s72-c/139136870_4fadd2f255.jpg
Kiumeni - WaulizeWanaume.
https://waulizewanaume.blogspot.com/2014/06/mambo-8-ya-kukumbuka-wakati-maisha-yako.html
https://waulizewanaume.blogspot.com/
http://waulizewanaume.blogspot.com/
http://waulizewanaume.blogspot.com/2014/06/mambo-8-ya-kukumbuka-wakati-maisha-yako.html
true
5715942833127633596
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy