Japo tabia, uongeaji na ucheshi huangaliwa zaidi na wanawake ila muonekano unachukua nafasi kubwa maana ndio utambulisho wako wa kwanza kwa mwanamke na zaidi ya hapo ndo unaokupa hadhi mbele ya mwanamke na kama umependeza ndivyo itafanya uongeze mvuto wako zaidi kwa mwanamke, hakikisha siku yako ya kwanza kukutana naye mfanye apendezwe na kuvutika zaidi na wewe kwa utanashati ulionao.
Kaka, ile sheria inayotumika wakati unataka kwenda mjini ndo hio hio inayotumika pia kama unataka wanawake wavutike na wewe, "kuwa mtanasharti na tunza usafi wako, kwa ufupi nenda ukaoge", muonekano wako hususani usafi wako na utanashati wako ndo utakufanya umpate huyo msichana unaemuwania maana jicho la kwanza atakalokua anakuangalia, akikuhisi unamtaka na umevutiwa naye huwa linaanzia utosini kwako mpaka miguuni kwako, atakutazama nywele zilivyokaa, atakuangalia shati lako na suruali yako uliyoivaa na jinsi zilivyo na mpaka kiatu chako kikoje.
Ukiuliza mwanaume yeyote yule kati ya mwanamke na mwanaume yupi ndie anaemchagua mwenzake, atakachokujibu ni kuwa mwanaume ndie anaechagua mwenza wake, ila ukiangalia kwa umakini na uelewa mkubwa wanawake ndio huwa wanaochagua wenza wao, maana kwa wastani mwanamke anaweza kuwa anatongozwa na wanaume kumi na akachukua muda wake kumchagua anayemtaka kati ya hao kumi ila kwa mwanaume mambo huwa ni tofauti anaweza kumchagua msichana amtongoze ila mambo yakaenda ndivyo sivyo, hii hali inaweza sababishwa hasa na muonekano mbovu wa kitanashati pamoja na kutozingatia usafi na kufanya mwanamke asikutilie maanani wala kukupa nafasi ya kukusikiliza na kufanya maneno yako mazuri kukosa mvuto.
Japo tabia, uongeaji na ucheshi huangaliwa zaidi na wanawake ila muonekano unachukua nafasi kubwa maana ndio utambulisho wako wa kwanza kwa mwanamke na zaidi ya hapo ndo unaokupa hadhi mbele ya mwanamke na kama umependeza ndivyo itafanya uongeze mvuto wako zaidi kwa mwanamke, hakikisha siku yako ya kwanza kukutana naye mfanye apendezwe na kuvutika zaidi na wewe kwa utanashati ulionao.
"Hili linaaminika, wanaume waliopendeza na walio na muonekano mzuri wa kisafi na kiutanashati huwa wanavutia zaidi wanawake na wanawake hupendezwa na kuvutika nao, huwa na urahisi mkubwa wa mafanikio katika mazungumzo na wanawake, hii inatokana kabla ya kumsemesha mwanamke, mwanamke anakuwa tayari katika hali ya kutaka kuongea naye".
Kiumeni.com inaendelea kukupa dokezo na kukuonyesha faida za muonekano mzuri kabla na wakati wa utongozaji na jinsi muonekano unavyoweza kutumika kuwavutia wanawake.
Ukiwa mtanasharti na muonekano wako upo katika hali ya usafi na unadhifu, hii hali inakufanya ujisikie upo katika hisia nzuri kifikra na kiakili, hii inakupa hali ya kujiamini na kukufanya uwe na mvuto wa uzuri na wa kupendeza kisura hata katika lugha yako ya kimwili na kama wote tunavyojua wanawake huchanganyikiwa na kuvutiwa sana na mwanaume anayejiamini.
Muonekano wa usafi unakurahisishia kazi ya kufanya mazungumzo na mwanamke, usafi na muonekano ulio makini humvutia hata mwanamke na kumfanya ajisikie hamu ya kuongea na wewe, utanashati unakupa hadhi, wanawake hupenda kuongea na mtu wanaodhania wao kwamba ana hadhi flani katika maisha, na ni rahisi kuongea na mwanamke iwapo na yeye anataka kuonge na wewe.
Kitu cha kwanza ambacho humvutia mwanamke kwa mwanaume ni utanashati wa mwanaume pamoja na jinsi huyo mwanaume anavyoonyesha kujiamini, mwanaume mtanashati huwavutia wanawake zaidi kuliko mwanaume aliyejiweka shaghara bagra na mchafu, ukiwa katika hali ya uchafu au kutokuwa nadhifu humfanya mwanamke asikupe nafasi ya kumsemesha na kujisikia vibaya kuongea na wewe na kuhisi kama anashusha hadhi yake kuongea na wewe mtu ambae hauna maana kwake.
"Kuvaa nguo ya gharama haimaanishi ndivyo utakavyopendeza zaidi, kupendeza hutokana na jinsi unavyofata mpangilio wa rangi na kuvaa kutokana na nyakati au sehemu uliyopo".
Kiumeni.com inaendelea kukuweka sawa kwa jinsi ya kuvaa ili uongeze mvuto wako zaidi na kumfanya mwanamke avutike na wewe, kutaka kuongea na wewe hata kabla hujamsogelea.
- #1, Fuata mpangilio wa rangi na vaa kutokana na rangi ya ngozi yako.
Kufuata rangi na mipangilio yake sio kwa wanawake pekee, wanaume tunaweza pia kufuatilia rangi, unaweza kupangilia kutokana na jinsi upendavyo na unaweza fanya majaribio tofauti tofauti mpaka ukapata rangi unayoona inaendana na wewe na kukupendezea zaidi, kwa wale wanaojiamini zaidi unaweza kufanya mpangilio mzuri wa rangi kutoka nguo ya nje mpaka zile za ndani.
Rangi huongeza mvuto na ukizipangilia kwa uzuri zitakufanya upendeze na uonekane mzuri wa sura na wakupendeza kwa wanawake hata kama una sura ngumu.
- #2, Vaa kulingana na mwili wako.
Usivae nguo kubwa sana au ndogo sana, nguo inatakiwa iendane na saizi ya mwili wako ili uweze kutokelezea na kupendeza kwa hali ya mvuto na utanashati zaidi.
- #3, Vaa vizuri ukizingatia nyakati na mahala ulipo.
Usivae tisheti kama unaenda kazini na usivae nguo ya kiofisi kama ukiwa unaenda mazoezini, zingatia sehemu ulipo na vaa kama inavyotakiwa.
- #4, Muonekano wa sura yako.
Kata nywele kulingana na umbo la kichwa chako, hakikisha sehemu zinazoonekana hasa usoni unaziweka nadhifu maana ndo sehemu ya kwanza mwanamke anayoiangalia wakati unamsogelea.
Tumia mafuta yanayoendana na ngozi yako kwa ngozi mororo na kuondokana na chunusi ili kukaa katika hali ya utanashati zaidi, kata kucha na jiweke katika hali ya kupendeza na kuvutia.
- #5, Tisheti.
Kila mwanaume anamiliki tisheti, ila wanaume wengi ambacho huwa
hawajui kuhusu hii nguo inaweza kukufanya upendeze sana kama ukiivaa
vizuri, tisheti inatakiwa iwe ndefu kiasi cha kufunika inchi tatu kutoka
kwenye mkanda wa ruxi na isiwe ndefu zaidi ya hapo, ikiwa ndefu zaidi
ya hapo itafanya uonekane muhuni na wanawake hawapendi wanaume wahuni,
iwapo ikiwa fupi itakuletea muonekano ambao usingependa.
- #6, Unadhifu.
Tunza muonekano wako kwa kuwa nadhifu, nyoosha na weka nguo zako katika hali ya usafi.
Unadhifu wako ndio hadhi yako na siku zote wanawake wanapenda mwanaume mwenye hadhi ya kuwa nao.
- #7, Viatu.
Kwa stairi yeyote ile unayoipenda, hakikisha vipo katika hali nzuri na vyenye umbo la kuvutia, viatu vya zamani vilivyo chakaa havitaweza kukuletea mvuto na unadhifu utakaokupa matokeo mazuri.
Viatu ukivipangilia rangi kuendana na nguo ulizozivaa vitakupendezesha katika hali ya kuvutia sana, jaribu kuwa na seti nyingi za viatu ili uweze kubadilisha kuendana na nguo zako.
Kiumeni.com imekuandalia orodha ya nguo na wakati wa kuzivaa ili kukuongezea mvuto zaidi na kukujengea hali ya kitanashati.
- Uvaaji wa kawaida ujumuishao tisheti, jinzi, kofia, kaptura na sendozi.
- Sherehe za kuzaliwa,
- Ufukweni,
- Pikiniki,
- Kwenda kuangalia filamu,
- Kwenda mpirani.
- Uvaaji nguo za kiofisi ujumuishao mashati, tai, suruali ndefu za vitambaa, viatu na vizibao.
- Msiba,
- Harusi,
- Sherehe,
- Kanisani.
COMMENTS